BACKGROUND


Nimeona ni vyema niandike Historia ya Maisha yangu japo kwa ufupi ili iwe ni Ushuhuda kwako utakao kutia moyo katika safari yetu hii ya kwenda mbinguni, Nilizaliwa tarehe 25/1/1982. Katika mkoa wa Kilimanjaro Tanzania. wakati huo mama yangu alikua anasoma katika shule ya msingi majengo moshi, mama yangu akiwa darasa la saba alipewa mimba na mwanafunzi mwenzake wa kidato kimoja aitwae Hassan Ally. mama yangu alipo mweleza juu ya swala hilo, kijana huyo alikataa na kusema mimba hiyo haikua yake, kutokana na hali ya ujauzito mama yangu alishindwa kuendelea na masomo. na wazazi wa mama yangu walikua ni wakali sana hivyo hawaku kubaliana na aibu ambayo mama alikua ameileta nyumbani, Muda wa kujifungua ulipo fika ndipo nilipo zaliwa,  nilipo fikisha myenzi michache wazazi wa mama walimfukuza mama na kumtaka anipeleke kwa baba yangu. mama yangu hakujua pa kwenda kwani hakua anapajua nyumbani kwa Hassani, hivyo aliamua kuchukua sumu na kupanga kujiua, akiwa amekaa katika kituo cha treni moshi na huku akiwa anafikiria jinsi ya kuanza kunywa sumu. moyoni akiwa anawaza aanze yeye kunywa sumu au ampe mtoto kwanza. ndipo alipo tokea mtu Mmoja [ nadhani alikua ni malaika ] na kumuuliza mbona umekaa kwenye jua kali na mtoto ?. ndipo mama alipo mwelezea yote yaliyo msibu  bahati nzuri mtu yule alikua anapafahamu nyumbani kwao kijana yule alie mpa mimba mama. hivyo aliamua kumpeleka, wazazi wa Hassani walipo mwona mama na walipo niona wali tupokea kwa furaha na walisema hii ni damu yao kwa sababu nilikua nafanana sana na baba yangu. hivyo baba hakua na lakusema. Bibi yangu mzaa baba alinipenda sana na wakaamua kuniita ALLY HASSANI ALLY, kwa sababu walikua ni waisilamu, tuliishi pale mpaka nilipoanza kutembea ndipo wazazi wa mama walipo muomba arudi nyumbani, hivyo mama alinichukua na tukarudi kwa Babu na bibi mpaka nilipo fikisha myaka saba, baba yangu pamoja na wazazi wake walihama  kutoka moshi mjini wakahamia Himo moshi, na Baba yangu akaoa mwanamke alieitwa Hadija,  Mwaka 1989, mama yangu aliamua kunipeleka Himo kwa baba yangu. huko himo nilijifunza uisilam na nikawa naswali katika msikiti wa Himo, mama yangu wa kambo alianza kunichukia sana Nakumbuka kila siku alikua ananiambia wewe ndo mtoto wa kwanza eeee ndo utarithi mali za baba yako eee, kwa kweli sikua naelewa maana ya maneno hayo, na kumbuka siku moja nikiwa nime jifanya kama nimelala nilimsikia akiwaambia watoto wake kwamba eti huyu Ally ndo atarithi mali za Baba yenu ?.  siku moja mchana mdogo wangu alichezea sabuni na kuilowesha mama yule alipo rudi alinipiga na Gongo kubwa sana kwenye bega kwa kweli sita sahau siku hiyo. nilikimbia sana na maumivu yalikua ni makali mno, ndipo Bibi yangu mzaa baba aliamua kunichukua tukawa tunaishi wote, bibi yangu alikua na hoteli ndogo ya kuuza chakula hivyo nikawa na msaidia wakati huo nilikua nimesha anza shule, nilizoma katika shule ya msingi himo. kisha baadae nikahamishiwa katika shule ya msingi makuyuni, nilikua na soma huku nikimsaidia bibi kuuza mandazi na sambusa. wakati mwingine nilikua natembeza mandazi na sambusa,  siku moja nikiwa ni melala na bibi yangu usiku wa manane ndipo ghafla nikashtuka na akatokea mtu akawa ana nikaba akitaka kuniua ndipo nika kumbuka kumwita yesu ambae nilishawahi kufundishwa na mama yangu. ghafla nikasikia kama kuna vita vikali sana  yule mtu aliekua ananikaba akaniachia na kukimbia. nilipoweza kuamka nikamwita bibi na kumwelezea bibi yangu alisema lala tu mjukuu wangu hilo ni jinamizi tu, kesho yake bibi yangu alinipeleka kwa mganga kupiga ramli mganga yule alisema hilo ni jini la kike limetumwa lije kumuua huyu mtoto. mganga yule alinichanja na kusema kwamba halita rudi tena. lakini usiku wa siku hiyo mambo yalizidi kua mabaya kwani ilipo fika saa ile ile. nika shtuka na yule mtu akaja tena kunikaba, kisha nikakumbuka kumwita yesu ambae mama yangu aliwahi kunifundisha habari zake, ghafla kukatokea vita vikali sana na lile jini lika niachia lika kimbia, kisha bibi yangu akanipeleka kwa yule mganga tena.  yule mganga akasema mtoto huyu ametumiwa majini na mama yake wa kambo ili ya muue kwa sababu yeye ndo atarithi mali za baba yake, mambo yalizidi kuwa mabaya sana na mama yule alikua ananichukia sana sikua najua kosa langu ni nini haswa, hivyo nikaamua kutoroka na kukimbilia Moshi mjini kwa babu na bibi wazazi wa mama yangu, wakati huo mama yangu alikua amesha olewa na anaishi arusha. nili mweleza bibi na babu mambo yaliyo nipata lakini hawaku nielewa. nilikaa moshi kwa babu nika amua kunza biashara ya kuuza biskuti na pipi na karanga pale moshi kwenye stendi ya mabasi. lakini matatizo  hayakuisha kwani usiku nilikua naona vitu vya ajabu wakati mwingine nilikua naona watu wananikaba. wakati mwingine nilikua naona picha za viumbe wa ajabu kwakweli hata siwezi kuelezea, bibi yangu alikua mkali sana akawa ananiambia nirudi kwa baba yangu. na kwa kweli nilikua naogopa kurudi kule hivyo bibi akawa ananifukuza ndipo mwaka 1996. nilipo amua kukimbilia Dar es salam. na kwakua sikua najua pakwenda niliamua kwenda katika kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha Dogo dogo Center. hapo nilipokelewa na kuanza maisha mapya nilikutana na watoto wengi sana, hapo nikakuta kuna Bendi ya muziki ya watoto iitwayo GREEN BAND, kwakeli nilivutiwa sana na jinsi walivyokua wanapiga muziki na nilitamani sana kujua kupiga guitar, nilijiunga na bendi hiyo na kuanza kujifunza kuimba. Mwalimu wa bendi alinipenda sana kwani nilikua na kichwa chepesi cha kuelewa muziki hivyo akaamua kunifundisha kupiga guitar la Bass. ndani ya muda mfupi nikaanza kupiga kwenye bendi, tukaanza kusafiri sehemu mbali mbali na tulikua tukialikwa kupiga muziki sehemu mbali mbali kwenye matamasha yanayo husu haki za watoto nak, tulifanikiwa kureko Santuri mbali mbali. moja ya nyimbo ambazo mpaka wa leo zinapigwa katika vituo mbali mbali vya Radio ni ule unao sema WATOTO WOTE WANA HAKI SAWA, mwalimu wa bendi aliyekua anaitwa Shedrak. aliamua kunifundisha kucheza guitar la rithim hivyo nikawa ndie mpiga rithim wa bendi. pia kulikua na kituo kingine cha sanaa ambacho kilikua kinakutanisha Watoto kutoka sehemu mbali mbali za Jiji la Dar es salam wanaoishi majumbani na wale wanaoishi mitaani kituo hiki kilikua katika maeneo ya FIRE Dare es salamu kilicho kua kinaitwa Anatoglo hapo nilikua nakwenda kila siku jioni kujifunza ngoma na maigizo katika kituo hiki nilikutana na wataalamu wa Muziki ambao walinisaidia sana haswa kwa upande wa upigaji Guitar na uimbaji hapo nilijifunza mambo mengi sana kuhusu Muziki, Baada ya kuiva kwenye muziki nilichukuliwa na jamaa mmoja aliekua anaitwa Bob chuwa tukaanzisha Bendi ya Muziki wa Reggae ambapo tulikua tunaishi maeneo ya Mbezi beach Dar es salam. nilidumu katika bendi hiyo karibu mwaka mmoja ndipo nilipokutana na dada mmoja aliyekua anaitwa Rehema huyu alinikutanisha na mzungu mmoja aliekua anaitwa Filipo ambae alinipeleka kwenye studio yake iliyokua maeneo ya Majumba sita ukonga. hapo nilikutana na Ras simba na marasta wengine wengi sana na kwasababu mzungu huyo alikua na vyombo vya Muziki tukaanzisha bendi ya Muziki wa Reggae iliyoitwa Tanzania rasta group ambapo tulifanikiwa kurekodi nyimbo kadhaaa zilizo tamba. moja ya nyimbo hizo ni Amani ulio kuwa unarushwa na TVT sasa hivi TBC, na ITV, wakati huo nilikua napiga guitar la solo, baada ya muda mzungu yule aliamua kurudi nyumbani kwao Finland, na ndipo maisha yalipoanza kuwa magumu kwani walio achiwa vyombo walianza kuuza chombo kimoja kimoja na ndipo bendi ikafa, baada ya muda nilihamia katika bendi ya Afrikan root liyokua chini ya Mwanamuziki Freedom balesija. hapo nilikutana na wapiga magitaa wengine ambao walinisaidia kujua muziki zaidi, nilikaa katika bendi hiyo kwa muda mfupi baadae nilijiunga na bendi ya Segere iliyokua maeneo ya kariakoo ambapo tulikua tukipiga nyimbo za kizaramo na taarab. baadae nilijiunga na bendi ya Bantu group iliyokua chini ya Hamza kalaa. nilikaa katika bendi hiyo kwa muda ndipo Mwaka 2002 nilipo kutana na Bob lau aliekua na Bendi pamoja na hotel katika mkoa wa Mbeya ambapo alinichukua na nikahamia Mbeya Tanzania, hapo nilijifunza mengi katika muziki hususan upigaji wa Guitar, nilikaa katika bendi hiyo mpaka mwaka 2003 mwishoni.   ndipo sikumoja nikasikia kwamba kuna mkutano wa injili uliokua umeandaliwa na kanisa la wasabato maeneo ya sokoine, niliamua kuhudhuria mkutano huo. kwakweli mahubiri yaliokua yanatolewa yalinivutia sana na nikaamua kununua Bibilia  yangu nikawa nasoma kila siku. kilasiku tulipokua tunakwenda kupiga muziki mimi sikua na Amani tena kwani niliwa katikati ya Muziki sauti ilikua ikiniambia je ingekuaje kama ungekua kanisani?, kwakweli sikua na Amani tena na nilitamani kuacha kazi hiyo. lakini changamoto iliyokua inanikabili ni kwamba kama nikiacha kazi ya muziki je nitaishije? kwani muziki ndio ulikua unanipatia mahitaji yangu ya kila siku,  katika mkutano ule niliamua kujitoa katika ubatizo lakini siku batizwa kwani siku ilipo fika nilikua nasafari ya kwenda moshi kusalimia Babu na bibi kwani ilikua imepita myaka mingi tangu nilipo ondoka. nilipo kua moshi nilitamani sana kwenda kumsalimia Baba yangu maeneo ya himo na nilipo kwenda nilikuta bibi yangu mzaa baba amesha fariki zamani. kwakweli nili sikitika sana. lakini kilicho nisikitisha zaidi ni kwamba nilikutana na mke wa Baba yangu mdogo na aliniambia maneno ambayo sita weza kuyasahau kamwe kwani alipo niona alishtuka sana [ kwani tulikua hatufahamiani ] aliniuliza wewe ndo Ally ? nilimjibu ndio na aliniambia wewe si walitaka kuku ua ? nikiwa mado nimeshikwa na butwaa aliniambia sikiliza mwanangu na kusihi sana usilale kwa baba yako leo na hatakama wakikupa chakula usile kwani mama huyo [ wakambo ] alidhamiria kukuua, baba yako alijaribu kuoa mke mwingine na wakazaa nae mtoto na mama yako huyo akamuua kwa uchawi hivyo mwanangu na kuomba usikubali kukaa hapa hata wakikupa chakula usile. kwakweli maneno yake yalinifanya nishangae sana, kwanza nilijiuliza huyu amejuaje mambo ambayo hata mimi nilisha yasahu zamani?. mama yangu wakambo aliponiona hakua na Amani kwani alikua na wasi wasi sana. na aliniambia nimsindikize kwa mama yake kuna kitu anataka kuchukua. tulipo kwenda mama yake aliniangalia kwa wasi wasi sana na ndipo mama yangu wa kambo alipo mwambia nimekuja kuchukua ile dawa . walionekana kua na wasi wasi na ndipo mama yake alipo sema nenda halafu uje kuchukua peke yako, tulirudi tena nyumbani na tulipo fika mama yangu wa kambo aliniambia Ally naomba usiondoke mpaka nije kwani narudi kwa mama kuchukua kitu fulani. mimi ndani yangu sikua na Amani sauti ikaniambia ondoka haraka urudi moshi kwa babu na bibi. nami siku kawia nikaondoka bila hata kuaga na kupanda gari kurudi moshi kwa babu, nilikaa kwa babu siku mbili na niliaga na kurudi Dar es salam ambapo nilirudi tena katika bendi ya Bantu Group iliyokua inaongozwa na Komandoo Hamza kalala.  Siku moja nikiwa naelekea maeneo ya Sinza kwaajili ya kujiandaa na onyesho la Usiku. nilipofika maeneo ya Sinza kijiweni niliona kibao kime andikwa KANISA LA WASABATO MANZESE. Nilimwomba rafiki yangu niliekua nae anipe kalamu nami nika paandika mahali pale na jina la Kanisa. Jumamosi iliyo fwata nilikwenda Kanisani wakati huo kwaya ya kanisa ilikua imesafiri imekwenda Nairobi kenya ila kulikua na waimbaji wachache waliokua wamebaki nilimuona Mmoja wao nami nikajitambulisha nikamweleza nia yangu. lakini alionekana ni kwamba hajali sana.baada ya ibada niondoka na niliendelea na shuhuli zangu za Muziki katika bendi ya Bantu Group. nako sikukaa sana baada ya muda mfupi nilijiunga na bendi ya Jupiter star, na nilirudi kuishi Kariakoo Dar es salam katika nyumba ambayo ndiyo yalikua maskani ya bendi ya Segere ambapo wanamuziki wengi walikua wanaishi hapo, Baada ya Muda Bendi ya segere walipata safari ya kwenda Kingoma kuburudisha katika siku ya wapenda nao [Valentine day] Na kwasababu nilikua naishi nao waliniomba nisafiri nao nika wapigie Guitar. nami nilikubali kisha tukaanza safari ambapo tulipanda Treni kutoka Dar es salamu kwenda Kigoma mjini. safari ilikua ni ndefu sana.  katika begi langu nilikua nime beba Bibilia yangu ambayo nili nunua nilipokua Mbeya,  ndipo nilipo anza kusoma Bibilia yangu. nilianza kusoma kitabu cha Ufunuo wa yohana nikajikua nakaribia kukimaliza nilipo fika Sura ya 18: 21 ndipo nilipo kutana na Maneno haya Kisha malaika mmoja mwenye nguvu sana akainua jiwe mfano wa jiwe kubwa la kusagia, akalitupa baharini akisema, "Ndivyo, Babuloni atakavyotupwa na kupotea kabisa.
 
Sauti za vinubi za muziki, sauti za wapiga filimbi na tarumbeta hazitasikika tena ndani yako. Hakuna fundi wa namna yoyote ile atakayepatikana tena ndani yako; wala sauti ya jiwe la kusagia haitasikika tena ndani yako.
 Maneno hayo yaliuchoma Moyo wangu kama mshale mkali sana nikajiona kwamba nimepote sana nami nikajiona kwamba namuhitaji Yesu kuliko chochote kile maishani. Baada ya kumaliza kusoma kitabu chote cha ufunuo wa yohana.  nilinyanyuka na kwenda dirishani nikawa nachungulia dirishani nilipo ona kwamba hakuna mtu anae niona ndipo nilipolia sana nikafanya Agano na Mungu. nikasema Ee Mungu ikiwa kama utanisaidia nifike salama huko ninako kwenda na ukinirudisha salama basi nitatafuta kanisa lolote utakalo niongoza nami nitakwenda na kukutumikia milele kuishi kwangu utajua wewe kila kitu nakikabidhi mikononi mwako,  Wanamuziki wenzangu walikua wakinishangaa sana kuniona na soma Bibilia nahali nilikua Muisilamu wengine waliniambia Ally unapotea sasa.  wengine waliona kwamba nina changanyikiwa. Lakini sikukata tamaa niliendelea kujifunza neno la Mungu na Roho wa Mungu aliendelea kunifundisha. 
Baada ya kurudi kutoka kigoma sauti iliniambia tena nirudi kule kanisani nilipokua nimekwenda mwanzo. nami nilikwenda mapema sana asubuhi nilipofika kanisani Moyo wangu ulishtuka sana nilipo muona Dk. Remi ongala  aliekua Mwanamuziki wa miziki ya kidunia akiingia kanisani. ndipo niliposema ikiwa kama Remi amejitoa kwa Yesu kwanini na mimi nisijitoe ? kisha nikawaona wapiga vyombo wakijaribu vyombo vyao. nilikaa kwenye kiti lakini baada ya muda mfupi sauti ile tena iliniambia nenda kule mbele wanako jaribu vyombo nawe ujitambulishe kwamba wewe ni mwanamuziki. nami nikatii nikaenda na kujitambulisha walionekana kwamba hawajali sana. nikarudi kukaa Baadae mmoja wawapigaji akaniambia njoo utujaribie Guitar. nami nikaenda nilipo anza kupiga walishituka sana kuona kwamba uwezo wangu wakupiga guitar uko juu sana vidole vyangu vilikua vyepesi sana. nilipomaliza kurekebisha guitar nilirudi nilipokua nimekaa. mara baada ya Ibada viongozi wa kwaya waliniita wakanza kuniuliza maswali. kwamba naishi wapi nami niliwaelezea ninapo ishi na kilicho nipeleka pale. walifurahi sana nao wakaniombea kisha wakanipa nauli nami nikaanza kuhudhuria mazoezi ya kwaya lakini bado nilikua naishi Kariakoo. nilijitoa kwa ubatizo kabla sijabatizwa kwaya ilipata safari ya kwenda Lushoto Tanga kwenye mkutano wa injili nami nikasafiri nao huko nikabatizwa kwa ubatizo wa Maji mengi na nikaamua kubadilisha jina langu na nikaitwa Amos na sasa jina langu kamili ni Prince Amos Mgeni kwa kweli sitasahau upendo walio nionyesha waimbaji wa kwaya ya Angaza. baada ya mkutano walinitafutia sehemu ya kuishi na sikurudi tena kule nilipokua naishi Mwanzo na huo ndio ukawa mwanzo wa huduma yangu katika Ufalme wa Mungu. nilipoanza kutumika kanisani nilipenda sana kumuimbia Mungu nilikua nikiwaona waimbaji wakiimba nyimbo za kumsifu Mungu moyo wangu ulikua unawaka kwa furaha nami nilitamani sana kuwa Muimbaji wa Muziki wa injili. siku moja tulisafiri na kwaya ya Angaza kwenda bunda musoma kwenye mkutano wa injili ambao ulikua umeandaliwa na Muinjilist Amon Mukangara. mahali ambapo tulikua tumepiga kambi kulikua na Mlima mkubwa ambao tulikua tunakwenda asubuhi kuomba. siku moja nilikwenda mlimani usiku peke yangu kumwomba Mungu kwakeli nilikua na ujasiri wa ajabu sana nami nika mwomba Mungu anipe karama ya kumwimbia yeye na kumtukuza. kwanzia siku hiyo nilianza mazoezi ya uimbaji Roho wa Mungu akaanza kuniongoza wakati mwingine nilikua naamshwa usiku na malaika kuomba.wakati mwingine nilikua nakwenda kanisani kukesha kisha napata wimbo mpya, Tangu nilipo jitoa kwa kazi ya Mungu nilikabiliwa na changamoto nyingi sana kwani nilijikuta sina kazi kwasababu kazi niliyokua nafanya mwanzo ya kupiga muziki kwenye bendi niliacha hivyo maisha yangu wakati mwingine yalikua magumu sana. lakini namshukuru Mungu kwani hakuniacha kwani Mungu amenipatia ujuzi na maarifa mbali mbali. na sasa mimi mbali na kuhubiri injili pia ni Mtayarishaji wa muziki wa injili yaani Producer Audio na video,  katika maisha yangu ya kiroho nimekabiliwa na changamoto nyingi sana nilipo amua kuachana na miziki ya kidunia shetani alinishambulia sana maisha yangu ya mekua na vita vikali sana kuna wakati nilianguka na kurudi nyuma kabisa. ulikua ni wakati mgumu sana katika maisha yangu nilipita katika kipindi kigumu sana. watu kwasababu hawajui kinacho endelea katika ulimwengu wa Roho na hawaoni kile nilichokua nakipitia katika ulimwengu waki roho watu walibaki kunihukumu na kunisema vibaya. lakini Yesu ambae anajua yote kunihusu mimi Yeye Mokozi hakuniacha kwani alinipigania na kuniinua tena nami nika amua kufanya maagano yangu upya na Yesu kwa Njia ya Ubatizo nami nikajitoa kwa ubatizo na Tarehe 10/12/2011 nikabatizwa Katika kanisa la Zimmerman Sda Nairobi Kenya nikaanza tena kumsifu Mokozi wangu alie nifia msalabani kwani yeye ndo anaejua thamani ya Roho yangu nami nimeweka nadhiri yakwamba nitamwimbia na kumtukuza Yeye peke yake siku zote za maisha yangu.

click hiyo player hapa chini usikilize wimbo unaozungumzia historia ya maisha yangu