PRINCE AMOS MINISTRY





                              PRINCE AMOS MINISTRY
Ni huduma ya Uimbaji Maombezi na Mafundisho ya Neno la Mungu. Mtumishi wa Mungu Prince Amos alipewa maono ya kuanzisha Huduma hii na mwaka 2006 akatoa Album yake ya kwanza Iliyoitwa Ee Baba pokea sifa ambayo ilikua na Nyimbo za kumtukuza Mungu pamoja na shuhuda za mambo makubwa Mungu aliyotenda katika Maisha yake. Prince Amos alianza kufanya Huduma hii katika mazingira magumu huku akikabiliwa na uhaba wa vitendea kazi na uhaba wa fedha. Kwani hali ya kiuchumi ilikua ni Ngumu sana. Hata pesa za kurekodi album ya kwanza Ilikua ni vigumu kuzipata Hivyo Prince Amos alianza kutafuta michango kwa watu mbali mbali Pesa kidogo aliyoipata ilimuwezesha Kurekodi Wimbo mmoja [Single] Ee Baba pokea sifa ambao ulianza Kurushwa katika kituo cha Radio cha Morning star. Kilichopo Dar es salam Tanzania.  Prince Amos aliendelea kuhangaika huku na kule kutafuta Pesa za kurekodi Album nzima ndipo Mungu akamuinua mtu mmoja aliejitolea kufadhili Urekodiwaji wa Album nzima. Baada ya kuhangaika sana Mungu alimpa Prince Amos maono ya kujifunza kazi ya Kurekodi Muziki Hivyo Prince Amos alianza kujifunza kazi hiyo na sasa yeye ni Producer Mtayarishaji wa Muziki wa Injili na Album zake zote Amekua akizirekodi mwenyewe,


LENGO LA HUDUMA


Lengo haswa la Prince Amos ministry nikuihubiri injili ya Milele kwa watu wote Kupitia Muziki wa Prince Amos watu wengi wame mpokea Yesu kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Nyimbo za Prince Amos zimejaa Sifa kwa Bwana, Shuhuda, Shukurani, Mafundisho na Uamsho wa Kiroho ukisikiliza Muziki wa Prince Amos utagundua kwamba nyimbo hizo zina mguso wa kipekee hii inatokana na maisha magumu na ya shida Prince Amos aliyoishi utotoni

MAOMBEZI


Prince Amos amekua akitoa Huduma ya maombezi kwa watu mbali mbali na Mungu ametenda miujiza mikubwa sana. Mungu amempa Prince Amos karama ya maombezi. na Muda mwingi wa maisha ya Prince Amos amekua akiutumia katika Maombi kwani maombi ndiyo ufunguo wakufungua hazina zote za Mbinguni 


MAHUBIRI


Prince Amos ministry inafanya Huduma ya kuhubiri injili Prince Amos anatoa mafundisho ya Neno la Mungu kwa kadiri Bwana alivyo mfunulia Nuru  hivyo Prince Amos anafundisha neno la Mungu kwenye Mikutano ya hadhara, Makanisani, Majumbani, na kwa mtu mmoja mmoja


MUZIKI


Prince Amos ministry inafundisha kupiga vyombo mbali mbali vya Muziki. kama vile Lead Guitar, Bass Guitar, Piano, Drams Nk. Prince Amos ministry inafundisha Uimbaji na namna ya kutunga nyimbo na kuandaa Muziki
pia Prince Amos Ministry inafundisha namna ya kua Mtayarishaji wa Muziki yani Music Producer 

AUDIO CD NA VIDEO CD
Kila baada ya mwaka mmoja au miwili Prince Amos hutoa Album mpya Audio. pesa zinazopatikana kutokana na mauzo ya kazi hizo hutumika kuhubiri injili pamoja nakusaidia wenye shida mbali mbali.
Pia Prince Amos huchagu nyimbo mbali mbali kutoka katika Albums zake za Audio na Kutengeneza Video Collection yenye nyimbo mchanganyiko kutoka katika Albums zake mbali mbali. Ambapo huitwa THE BEST OF PRINCE AMOS VIDEO COLLECTION 1 2 3 4 5 NK. 

P.A.PRODUCTIONS
P.A.Productions ni kampuni [Studio] ndani ya Prince Amos Ministry ambapo kazi yake ni Kurekodi Muziki wa Injili Audio na Video kwa Garama nafuu ili kusaidia waimbaji mbali mbali wa Muziki Huo [ COMING SOON

PRINCE AMOS GOSPEL MUSIC CENTER 
Hili ni Duka linalo uza na Kusambaza kazi za Prince Amos pamoja na kazi za waimbaji wengine wa Muziki wa Injili. Duka hili huuza na kusambaza AUDIO CD, DVD, VICD pamoja na VITABU Mbali mbali vya Neno la Mungu [COMING SOON]